Friday, June 7, 2013

Anfield kuongezwa hadi kufikia watazamaji 60,000

Upgrade: The 45,000-seater stadium will be extended once planning permission is accepted
Klabu ya Liverpool ipo kwenye hatua za mwisho kufanikisha mpango wake wa kupanua uwanja wa Anfield ili kufikia idadi ya watazamaji 60,000 kutoka 45,000 hivi sasa. Lengo kuu la kutanua uwanja huu ni kuongeza mapato ili klabu ya Liverpool iweze kupata mapato ya kuiwezesha kushindana na klabu zingine kubwa kiuchumi, zaidi katika uwezo wa kununua wachezaji wakubwa na kuweza kuwalipa mishahara mikubwa. Mpango huu umekuja baada ya kughairisha mpango wa kujenga kiwanja kipya sehemu nyingine licha ya kuwa mpango huu wa kutanua kiwanja hadi sasa umeshindikana kuanza kwasababu nafasi ya utanuzi ni ndogo na baadhi ya wamiliki wa nyumba za jirani wametaka kulipwa pesa nyingi ambazo zipo nje ya bajeti ya klabu hiyo. Ila uongozi wa Liverpool umesema wataendelea kuwashawishi wamiliki hao wa nyumba za jirani hadi kufikia muafaka na kuzinunua nyumba hizo. Mipango yote ikienda kama ilivyopangwa kazi ya kutanua uwanja inatarajiwa kuanza mwishoni mwa msimu ujao. Hadi sasa nchini Uingereza kiwanja cha Man utd Old Trafford ndicho kina uweza wa kubeba watazamaji wengi kuliko vingine kwenye ngazi ya vilabu, kwani uwanja huo unabeba watazamaji 76,212, ikifuatiwa na Uwanja wa Arsenal, Emirates watu 60,355, Uwanja wa Newcastle 52,454 na Man city 47,805.  

No comments:

Post a Comment