Sunday, June 9, 2013

Madrid yaikatisha tamaa United kumrudisha Ronaldo

Klabu ya Man utd ipo kwenye wakati mgumu kumrudisha mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo baada ya mchezaji huyo kutoa ahadi ya kusaini makubaliano mapya na Real Madrid. Ronaldo aliyasema hayo usiku wa kuamkia leo alipokutana na mmoja wa maofisa wa Man utd aliyetumwa kufuatilia usajili wake. Ofisa huyo alimnukuu Ronaldo akisema ‘kwasasa nimetulia, naamini tunaelekea kufikia muafaka kati yangu na Real Madrid ili kusaini mkataba mpya, kwa hili lazima nisema ukweli, wakati wowote tutakubaliana na nitaendelea kuwa mchezaji wa Madrid”. Kufuatia kauli hiyo ya Ronaldo, Ofisa huyo wa Man utd alisema “sisi tumekata tamaa, kwasababu tulikuwa tumepanga kulipa ada ya dola mil 65 kumsajili Ronaldo na kumlipa paundi 300,000 kwa wiki na angekuwa mchezaji anayelipwa kuliko wote Uingereza, lakini wenzetu wa Madrid wameahidi kumlipa paundi 500,000 kwa wiki pamoja na asilimia 40-60 ya haki miliki yake kwenye vyombo vya habari, hivyo tunangojea kuona nini kitaendelea”. Hatua hii imefanya klabu ya Man utd kukata tamaa ya kumrudisha Ronaldo Old Trafford na kuharibu mipango yote iliyopangwa na Man utd kuweza kumtangaza rasmi mchezaji huyo August 8.  

No comments:

Post a Comment