Klabu ya Liverpool imetangaza kuonesha live mechi kati ya Uruguay na Jordan kupitia kituo cha luninga cha klabu hiyo LFCTV. Klabu ya Liverpool imesema imechukua uamuzi wa kuonesha live mechi hiyo ili kuwapa raha mashabiki wa klabu hiyo kwa kumuangalia mchezaji wao kipenzi Luis Suarez. Mechi hii itakuwa ni ya marudiano kuwania kufuzu kombe la dunia mwakani baada ya mechi ya kwanza iliyochezwa wiki hii, ambapo Uruguay walishinda magoli 5-0 dhidi ya Jordan. Mechi ya marudiano itachezwa jumatano ya tarehe 20 Novemba.
No comments:
Post a Comment