Team | MP | W | D | L | GF | GA | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|
Argentina | 13 | 7 | 5 | 1 | 25 | 9 | 26 |
Colombia | 12 | 7 | 2 | 3 | 21 | 7 | 23 |
Ecuador | 12 | 6 | 3 | 3 | 17 | 12 | 21 |
Chile | 13 | 7 | 0 | 6 | 21 | 21 | 21 |
Uruguay | 12 | 4 | 4 | 4 | 18 | 21 | 16 |
Venezuela | 13 | 4 | 4 | 5 | 10 | 14 | 16 |
Peru | 12 | 4 | 2 | 6 | 12 | 17 | 14 |
Bolivia | 13 | 2 | 4 | 7 | 15 | 24 | 10 |
Paraguay | 12 | 2 | 2 | 8 | 9 | 23 | 8 |
Kulingana na msimamo huu kila timu imebakiza mechi 3 na 4, na kutoka kwenye bara hili la Amerika ya kusini timu nne (4) tu ndiyo zinatakiwa kushiriki kwenye fainali za kombe la dunia. Timu itakayomaliza kwenye nafasi ya tano itacheza playoff na timu moja kutoka bara la Asia ambayo pia itakuwa kwenye nafasi ya tano, mshindi kwenye mechi hiyo ndiye ataingia kwenye fainali nchini Brazil. Katika msimamo huu hadi sasa timu ya taifa ya Paraguay imeshajitoa kwenye michuano hiyo baada ya kufungwa michezo mingi, na ikumbukwe kuwa timu hii ya Paraguay ilifikia hatua ya robo fainali kwenye fainali za kombe la dunia nchini Afrika ya Kusini baada ya kutolewa kwa tabu na Spain kwa goli moja. Paraguay imefikia kwenye hali hii kwa kile kinachoelezwa kuwa bara la Amerika ya kusini ndiyo lina ushindani mkubwa kuliko mabara yote katika kufuzu kuingia kombe la dunia. Pia nchi ya Brazil kuandaa michuano hii kumesaidia kundi hili kupunguza ushindani kwani Brazil imepata tiketi ya ushiriki kwenye fainali hizo moja kwa moja ikiwa ni nchi mwenyeji.
No comments:
Post a Comment