Mkongwe wa soka duniani Romario (Mbrazil) jana alitoa machozi alipokuwa akiongelea hali ya maisha ya watu wa Brazil ikilinganishwa na matumizi ambayo serikali ya Brazil inayafanya kuandaa kombe la dunia. Romario alisema anaungana na waandamanaji wote wanaopinga Brazil kuandaa kombe la dunia kwa kutumia gharama kubwa wakati huduma za muhimu za kijamii ni duni ndani ya nchi hiyo. 'Siamini kama kombe la dunia litaleta nafuu ya maisha Brazil, wananchi wana maisha magumu sana, ni bora fedha hizi zinazotumika kuandaa kombe la dunia zingetumika kuwapatia wananchi mahitaji yao muhimu' hayo yalikuwa ni maneno ya Romario. Taarifa hizi zimekuja baada ya kundi kubwa la waandamanaji wapatao milioni moja nchi nzima kuandamana wakipinga kufanyika kwa michuano ya kombe la mabara na dunia nchini Brazil. Nukuu: Serikali ya Brazil imetenga kiasi cha paundi bilioni 26 kwa ajili ya michuano hii. |
Tuesday, June 25, 2013
Romario atoa machozi kuhusu hoja ya waandamanaji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment