Tuesday, June 11, 2013

Siwezi kumpendelea Terry wala Lampard - Mourinho

Kocha mpya wa Chelsea Jose Mourinho jana alitambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari kama kocha mpya wa Chelsea, moja ya maswali aliyojibu ilikuwa ni kuhusiana na wachezaji wake wa zamani aliowaacha Chelsea akiwemo Terry na Lampard, waandishi walipenda kujua kama wachezaji hawa watapata upendeleo kwasababu wametoka mbali na wameitumikia Chelsea kwa muda mrefu, Mourinho alijibu kwa kusema ‘ hakutakuwa na upendeleo wowote kwa wachezaji hawa, wananijua nilivyo sina haja ya kuwaambia wao tabia yangu kwasababu wananijua vyema, ila ni vyema nikawaambia nyinyi (waandishi) ili mnifahamu pia. Lazima niseme ukweli, kama mchezaji anatakiwa kucheza na ana uwezo wa kucheza kwenye kila mechi nitampanga, ila kama hana uwezo wa kucheza siwezi kumpanga eti tu kwasababu ya mahusiano yetu ni mazuri au kwasababu anapendwa na watu, daima nitakuwa nafanya maamuzi ya kisoka bila ya upendeleo wowote’. Mbali ya haya Mourinho pia aliongelea masuala mengine kuhusu mipango yake ya misimu ijayo, unaweza kumsikiliza kwa kubofya hapa

No comments:

Post a Comment