Wednesday, May 1, 2013

Barcelona yaendeleza uteja kwa Bayern Munich

Timu ya Barcelona imendeleza uteja kwa Bayern Munich baada ya kukubali kipigo cha goli 3-0 na kufanya itolewe kwa jumla ya magoli saba kwa bila. Idadi hii ya magoli ni ya kihistoria kutokea katika michuano ya UEFA katika hatua ya nusu fainali. Vilevile ndani ya klabu ya Barcelona kichapo hiki ni cha kihistoria na kitaweza kudumu kwa miaka mingi. Mapungufu yale yale yaliyojitokeza Ujerumani ndiyo yaliyoifanya Barca kupigwa tena wakiwa nyumbani, kukosekana kwa mabeki wake mahiri kina Mascherano, Puyol, Abidal na Busquets kulifanya ngome ya Barca kupwaya sana kiasi cha kuwafanya washambuliaji wa Bayern kucheza wanavyotaka. 

Mechi ya leo Barcelona walishaiona ngumu tokeo Ujerumani baada ya kupigwa goli nne, ndiyo maana benchi la ufundi halikuona umuhimu wa kufanya jitihada za kuwawezesha Messi, Busquets na Abidal kucheza. Vilevile, kocha aliwatoa Xavi na Iniesta kipindi cha pili ili kuwapa nafasi wachezaji wengi ambao mara kwa mara hucheza kama kikosi cha pili. Nusu fainali hii imeiweka Hispania katika aibu kubwa kwani Real Madrid na Barcelona ndiyo vilabu nyota vya nchi hiyo lakini zimetolewa na kwa mpigo na klabu za nchi moja, nchi ambayo kiubora wa soka ipo nafasi ya pili kwenye renki za FIFA wakati wao Hispania wakiwa nafasi ya kwanza. 

Barcelona na Real Madrid ndiyo kwaheri mwaka huu kwenye UEFA champions na ubaya zaidi michuano hii ya UEFA haina kikombe cha mshindi wa tatu kombe ambalo lingetumika kutuliza maumivu ya Barca na Real, hivyo huu ni muda wa kujipanga tena kwa msimu ujao. Fainali ya mwaka huu itakayofanyika nchini Uingereza kwenye moja kati ya viwanja bora duniani Wembley itakuwa ni kati ya Bayern Munich na Borussian Dortmund. 

Hamstrung: Lionel Messi (right) was left on the bench despite Barca's need to overturn a four-goal deficit
Messi alikuwa benchi mwanzo mwisho, ila sura yake ilikuwa inaonesha hajafurahia uamuzi wa kocha wake kumuweka benchi, ila ukweli hata angeingia hakuna kitu angeweza kufanya ni bora alivyopumzika kuepusha maumivu zaidi kwenye mguu wake
'Proud of Barca!': Barcelona's fans packed out the Nou Camp in the hope of seeing a comeback
Uwanja ulifurika na kupendezeshwa na rangi nzuri lakini mwisho wake ilikuwa ni kilio
Fussball's coming home: Bayern secured an all-German Champions league final against Borussia Dortmund
Bayern wakishangalia goli la Robben
Hang your head: Barca goalkeeper Victor Valdes screams in frustration after Pique's gaffe
Pique na Valdes wakiwa hawana la kufanya baada ya goli la pili kuingia 

No comments:

Post a Comment