Ronaldo-Man utd
Sir Alex ametajwa na vyombo vya habari kuwa amepewa kazi ya kuongea na Cristiano Ronaldo ili kumshawishi kurudi United. Ronaldo mwenye ameshaonesha nia ya kurudi United kwa kile kinachosemekana ni kuwa na mahusiano mabaya na baadhi ya viongozi wa Madrid, lakini kipingamizi kikubwa ni uongozi wa Madrid ambao hadi sasa wamegoma kumruhusu Ronaldo kujiunga na United licha ya kuwa Man utd wamesema wapo tayari kutoa kiasi cha paundi mil 80 au zaidi kumsajili Ronaldo. Ila wadau wengi wa soka wanaamini kuwa Madrid watamuachi Ronaldo dakika za majeruhi ila kwa bei kubwa.
Henrikh-Liverpool
Klabu ya Liverpool ipo kwenye hatua za mwisho kumnasa kiungo wa Shakhtar Donetsk Henrikh Mkhitaryan kwa kiasi cha paundi mil 17. Henrikh mwenye umri wa miaka 24 ameweza kuwavutia Liverpool baada ya kuonesha mchezo mzuri kwenye mechi ya kuwania kufuzu kombe la dunia ambapo timu yake ya taifa (Armenia) ilishinda magoli 4-0 dhidi ya Denmark na yeye akiwa ndiye chachu ya ushindi kwa kucheza vyema kwenye nafasi ya kiungo. Liverpool wameshaanza mazungumzo na klabu ya Shakhtar na taarifa za awali zinasema uwezekano wa kumsajili ni mkubwa.
Valdes-Monaco
Klabu ya Monaco ya Ufaransa ipo kwenye mazungumzo na golikipa wa Barcelona Victor Valdes ili aweze kujiunga na klabu hiyo kwa misimu ijayo. Valdes ambaye amemaliza mkataba wa kuichezea Barcelona msimu huu, aligoma kusaini mkataba mwingine na klabu hiyo akisema anahitaji kwenda sehemu nyingine ili kubadilisha mazingira. Mbali ya Monaco, klabu ya Arsenal pia imeonesha nia ya kumsajili Valdes licha ya kuwa Monaco ndiyo wapo kwenye mazingira mazuri ya kumnasa Valdes kutokana na uwezo wao wa kifedha kuwa mkubwa.
Reina-Barcelona
Kufuatia taarifa za Victor Valdes kuhama Barcelona, klabu hiyo ipo kwenye harakati za kutafuta mbadala wa Valdes na hadi sasa mazungumzo yanaendelea ili kumsajili golikipa wa Liverpool Pepe Reina licha ya kuwa klabu ya Liverpool haijawa tayari kumuuza Reina. Mbali ya Reina Barcelona pia wamehusishwa kumsajili golikipa wa Malaga Wilfredo Caballero baada ya kuonesha uwezo mzuri msimu uliopita kwenye ligi na klabu bingwa Ulaya.
Radu-Man city
Klabu ya Man city imehusishwa kumsajili mlinzi wa Lazio ya Italia, Stefan Radu ili kuweza kuongeza nguvu baada ya Kolo Toure kuhamia Liverpool. Man city imetoa ofa ya kuwapatia Lazio wachezaji wawili Lescott na Kolarov ili wamsajili Radu, lakini tetesi zinaonesha kuwa Lazio watakataa kwani mchezaji wao ana thamani ya paundi mil 15.
Fabregas-Man utd
David Moyes bado hajakata tamaa ya kumsajili Cesc Fabregas wa Barcelona baada ya klabu hiyo kuonesha nia ya kumuuza mchezaji huyo baada ya kupata wakati mgumu wa kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha Barca. Man utd wamejiandaa kutoa dau la paundi mil 25 kwa mchezaji huyo licha ya kuwa Fabregas mwenyewe alisema hawezi kuhama Barcelona kwasababu ni ndoto yake ya miaka mingi kuchezea Barcelona. Moyes anamuhitaji Fabregas ili kutatua tatizo kwenye nafasi ya kiungo, kwasababu msimu uliopita Rooney hakuweza kucheza vyema na Scholes amestaafu.
Bale-Madrid
Real Madrid na Tottenham bado wapo kwenye mazungumzo yasiyofikia muafaka kuhusu uhamisho wa Gareth Bale. Kikwazo kikubwa cha usajili wa Bale kwenda Madrid ni kocha wa Tottenham AVB ambaye anamshawishi Bale asihame kwani anafahamu kuwa mchezaji huyo ndiye chachu ya ushindi kwa Tottenham. Rais wa Madrid Perez alitamka hadharani kuwa Madrid ipo tayari kutoa kiasi chochote cha fedha ili kumsajili Bale na fedha hizo tayari amepewa Zinedine Zidane ambaye ni muakilishi wa klabu hiyo kwenye usajili wa Bale. Lakini hadi sasa usijili wa Bale bado ni mgumu kutokana na vikwazo vya klabu ya Tottenham ila historia inaonesha klabu ya Madrid ikimuhitaji mchezaji lazima itamnunua tu, tuendelee kungojea kuona vita hivi vya Tottenham na Madrid vitafikia wapi.
AVB-PSG
Baada ya kocha wa PSG Carlos Ancelotti kutamka kuwa anataka kwenda Madrid, klabu ya PSG imeanza mazunguzo na kocha wa Tottenham Andre Villa Boas (AVB) ili kuziba pengo la Ancelotti lakini hadi sasa uhamisho huu una mashaka kwani AVB mwenyewe bado hajaonesha nia ya kuhamia PSG kutokana na maendeleo mazuri ya timu yake (Tottenham) na mipango aliyojiwekea kwa Tottenham. Ila uwezo mkubwa wa kifedha PSG iliyonao unaweza kubadilisha mawazo ya AVB na kuhamia Ufaransa.
Isco-Man city
Baada ya Pellegrini kutangazwa kuwa kocha mpya wa Man city akitokea Malaga, klabu ya Man city bado inaendelea kutekeleza mapendekezo ya kocha huyo ikiwemo kumsajili kiungo wa Malaga Isco. Isco ambaye ni mchezaji tegemezi wa Malaga na kipenzi wa Pellegrini limeufanya uongozi wa Man city kukubali kutoa pesa ili mchezaji huyo asajiliwe jambo ambalo litarahisisha kazi ya Pellegrini kuitengeneza Man city ili kucheza mchezo unaotaka kufanana na Malaga. Na taarifa zinasema, kutokana na hali ngumu ya kiuchumi kwa klabu ya Malaga, klabu hiyo ipo tayari kumuachia Isco kwa paundi mil 30 ili ajiunge na Man city.
Higuain-Arsenal
Klabu ya Arsenal pia bado ipo kwenye mazungumzo na Madrid ili kumsajili Gonzalo Higuain. Tetesi za Higuain kuhamia Arsenal zimeanza wiki mbili zilizopita na tatizo kubwa lililopo hadi sasa ni ugumu wa klabu ya Arsenal kutoa pesa ambazo Madrid wamehitaji ili kumsajili mchezaji huyo. Madrid wamehitaji paundi mil 25 lakini Arsenal wao wapo tayari kutoa kiasi cha paundi mil 15 jambo ambalo limefanya usajili wa mchezaji huyu kushindikana hadi leo. Kuchelewa kukubaliana kati ya klabu hizi mbili kumeanza kuleta nuksi kwa Arsenal kwani hadi sasa klabu za PSG, Chelsea na Monaco zimesema zipo tayari kilipa zaidi ya Arsenal ili kumsajili mchezaji huyo na Higuian mwenye yupo tayari kwenda popote kwani alishasema msimu ujao hatakuwepo Madrid. 'Wenger kweli mchumi :) '
Koscielny - Barcelona
Klabu ya Barcelona imetoa ofa ya paundi mil 20 kwa Arsenal ili kumsajili beki wa kati Laurent Koscielny. Ofa hiyo ya Barca imekuja siku chache baada ya Koscielny kuonesha nia ya kuhama Arsenal baada ya kuongea kwenye vyombo vya habari kuwa anahitaji kucheza kwenye klabu ambazo ataweza kushinda vikombe na kujenga historia nzuri kwenye maisha yake ya soka. Lakini hadi sasa Arsenal bado hawajajibu lolote kwa Barcelona kuhusiana na ofa hiyo na taarifa za awali zinaonesha Arsenal haipo tayari kumuuza Koscielny pamoja na wachezaji wengine wakubwa ndani wa klabu hiyo lengo ni kuijenga upya Arsenal ili irudi kwenye hadhi yake ya zamani
Jovetic-Chelsea
Kocha mkuu wa Chelsea Jose Mourinho ameitaka klabu hiyo kufanya usajili wa Stevan Jovetic haraka iwezekanavyo ili aanze kupanga kikosi chake. Jovetic ambaye alikuwa ni chaguo la Arsenal, usajili wake umeibiwa na Chelsea kutokana na fedha kidogo ambazo klabu Arsenal ilitoa kwa Fiorentina. Tayari mkurugenzi wa masuala ya usajili wa Fiorentina Daniele Prade amekutana na wakala wa mchezaji huyo Vlado Lemic na Giuseppe Riso ili kufanikisha uhamiso wa Jovetic na taarifa zinasema mazungumzo hayo yamefanikiwa hivyo wakati wowote mchezaji huyo atawasili darajini kwa vipimo na kusaini mkataba kama mambo yote yatakwenda yalivyopangwa.
Jovetic-Chelsea
Kocha mkuu wa Chelsea Jose Mourinho ameitaka klabu hiyo kufanya usajili wa Stevan Jovetic haraka iwezekanavyo ili aanze kupanga kikosi chake. Jovetic ambaye alikuwa ni chaguo la Arsenal, usajili wake umeibiwa na Chelsea kutokana na fedha kidogo ambazo klabu Arsenal ilitoa kwa Fiorentina. Tayari mkurugenzi wa masuala ya usajili wa Fiorentina Daniele Prade amekutana na wakala wa mchezaji huyo Vlado Lemic na Giuseppe Riso ili kufanikisha uhamiso wa Jovetic na taarifa zinasema mazungumzo hayo yamefanikiwa hivyo wakati wowote mchezaji huyo atawasili darajini kwa vipimo na kusaini mkataba kama mambo yote yatakwenda yalivyopangwa.
No comments:
Post a Comment