Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara 2012/2013 Young Africans ambao pia ni Mabingwa watetezi wa kombe la Kagame. jumatatu wanatarajia kuanza mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola Mabibo kujiandaa na mashindano ya kombe la Kagame yanayotarajia kuanza Juni 18 mwaka huu nchini Sudan. Katika mashidano ya mwaka huu nchini Sudan , Yanga imepangwa katika kundi C lenye timu za Express FC (Uganda), Vitaloo FC (Burundi) na Ports FC (Djibout) ambapo kundi hili litakua katika mji wa El Fashir Kaskazini mwa jimbo la Darfur. Yanga itaanza kutetea ubingwa wake Juni 20 dhidi ya timu ya Express ya Uganda, kisha Juni 22 itacheza na Ports ya Djibout kabla ya kumalizia mchezo wake wa mwisho katika makundi dhidi ya timu ya Vitaloo Juni 25 michezo yote ikifanyika katika uwanja wa El Fashir. Young Africans ambayo ilitwaa ubingwa wa VPL ikiwa na michezo miwili mikononi inaanza mazoezi jumatatu asubuhi kuhakikisha inajiandaa vema kwenda kushindana na kurudi na kombe hilo kwa kulitwaa kwa mara ya tatu (3) mfululizo, ambapo mpaka sasa imeshalitwaa mara 5.
No comments:
Post a Comment