![]() |
Imesemekana klabu ya Chelsea imehamishia majeshi yake ya usajili kwa Wayne Rooney na Robert Lewandowski baada ya klabu ya PSG kutoa ofa kubwa zaidi ili kumnasa mshambuliaji wa Napoli Edinson Cavani. PSG wametoa ofa ya paundi mil 43 kwa Napoli ili kumsajili Cavani, pesa ambazo ni juu ya dau la Chelsea na Man city. Kutokana na ushindani huu, klabu ya Chelsea imeelekeza nguvu zake kumsajili Rooney au Lewa, wachezaji ambao wanaaminika kuwa uwezo wao hautofautiani sana na Cavani. Lakini taarifa za vyombo vya habari zinasema, Chelsea bado ipo kwenye wakati mgumu pia kuwasajili wachezaji hawa (Rooney na Lewa) kutokana na ukweli kwamba klabu zao hazipo tayari kuwaruhusu waondoke. Kwa upande wa Rooney, wiki hii kocha wa Man utd alikutana na Rooney kwenye kikao ambacho kilikuwa ni cha siri na hadi sasa haijajulikana walikubaliana nini, lakini mazingira yalivyo inaonesha kuwa Rooney na Moyes wamefikia muafaka mzuri. Upande wa Lewandowski, mchezaji huyu aliomba kuhama Dortmund kwenda Munich mara tu fainali za Uefa zilipomalizika, lakini uongozi wa klabu yake ukasema Lewa sio mchezaji wa kuuzwa na ataendelea kubaki Dortmund. Kwahivyo, mazingira haya ndiyo yanafanya kuwe na ugumu kwa Chelsea kuwapata wachezaji hawa, ila lolote linaweza kutokea kwani msimu wa usajili bado unaendelea na mapinduzi yanaweza kufanyika, tuendelee kusubiri hadi dakika 90 za usajili zitakapofika. |
Tuesday, July 2, 2013
Chelsea imehamishia majeshi kwa Rooney na Lewa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment