Michezoupdates imefanya utafiti kwa kuhesabu idadi ya washabiki kwa klabu kubwa barani Ulaya ambao wamelike page rasmi ya Facebook ya klabu hizo. Matokeo ya utafiti huu yamefanywa tarehe 19 mwezi Julai 2013, hivyo siku yoyote baada ya hapa idadi inaweza kubadilika, lakini matarajio ni kwamba tarakimu kuu za mwanzo zitaendelea kuwepo kwa kipindi kirefu kidogo. Katika tafiti hizi, Michezoupdates imebaini kwamba, klabu kuwa na likes nyingi za Facebook haimaanisha kuwa klabu husika ina washabiki wengi kuliko nyingine duniani, bali likes nyingi ni ishara ya kuwa maarufu kuliko klabu zingine duniani. Tafiti hii imebaini FC Barcelona na Real Madrid ndiyo zenye likes nyingi kwa tofauti kubwa dhidi klabu zingine na kwa mujibu wa Michezoupdates, sababu kubwa zinazosababisha klabu hizi mbili kuwa na likes nyingi, ni kuwa na wachezaji maarufu ambao hupendwa na wapenda soka wengi duniani kama Cristiano Ronaldo na Lionel Messi. Wachezaji hawa pekee wana likes nyingi kuliko klabu zao, hii ni kuonesha kuwa wao ni maarufu kuliko klabu zao, ambapo Cristiano Ronaldo hadi sasa ana likes 59 milioni na Messi 47 milioni, hii ni sababu tosha kuzifanya klabu zao pia kupata likes nyingi kupitia wao. Nchini England, klabu ya Man utd imewazidi wapinzani wake mara mbili zaidi kwa idadi ya likes za facebook, hii inamaanisha kuwa Man utd ni maarufu zaidi duniani kwasasa kuliko klabu za Chelsea, Arsenal, Liverpool na Man city, kwani kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2000 hadi sasa 2013 imeweza kushinda kombe la ligi mara saba, wakati Chelsea mara tatu na Arsenal mara mbili tu ikizingatiwa kuwa ligi ya Uingereza ndiyo maarufu kuliko zote duniani. Kwa upande wa Liverpool ushindi wa klabu bingwa Ulaya mwaka 2005 na ushindani iliyonayo dhidi ya klabu kubwa za England na Ulaya ndiyo umeifanya iongeze umaarufu zaidi duniani. Wakati klabu za ligi nyingine zimeonekana kuwa na likes ndogo kutokana na ligi zake kutokuwa maarufu na uchache wa wachezaji wanaojulikana kwenye ligi hizo. Ifuatayo ni orodha kamili ya timu na idadi ya likes hadi leo hii tarehe 19 Julai 2013.
Kwa klabu za bongo ni kama inavyojionesha
Timu
|
Likes Facebook
|
Simba
|
26,229
|
Yanga
|
13,708
|
Azam FC
|
12,880
|
No comments:
Post a Comment