Uongozi wa matawi wa klabu ya Yanga (wenyeviti na makatibu) leo umefanya kikao katika makao makuu ya klabu mtaa wa twiga/jangwani kisha kutoa tamko lao kwa waandishi wa habari kuhusiana na tamko la uongozi (kamati ya utendaji) kutokubali kuonyeshwa kwa michezo yake kwenye luninga. Awali klabu ya Yanga juzi kupitia kamati ya utendaji ilifanya mkutano na waandishi wa habari juu ya mustakabali wa klabu kuhusiana na kutoridhishwa na kamati ya muda ya Ligi (TPL) kuingia makubaliano ya kurushwa matangazo ya televsheni kwenye michezo yake. Akiongea na waandishi wa habari leo katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako alisema baada ya kukaa na viongozi wa matawi ya klabu ya Yanga jijni Dar es salaam kwa pamoja wamekubali na kuunga mkono hoja zilizowasilisha na viongozi juu ya haki ya matangazo. Mmoja wa viongozi wa matawi Bakili Makele akiongea kwa niaba ya viongozi wa matawi, alisema TFF inaamua kukandamiza soka la Tanzania kwa kuviamulia maamuzi yake juu ya kuonyeshwa kwa michezo ya timu kwenye luninga. Makele amesema taratibu za kuipa kampuni ya Azam TV tenda ya kuonyesha michezo ya Ligi Kuu haikua na usawa, kampuni hiyo bado haijaanza hata matangazo, haijulikani ofisi zake zilipo, uwezo wa kurusha matangazo haujulikani kwa watanzania lakini bado wamepewa nafasi hyo. Kikubwa tunamuomba rais wa TFF Leodgar Tenga kulitazama suala hili kwa umakini, kwani mtazamo wetu viongozi wa kamati ya Ligi wametazama maslahi yao binafsi bila kuzingatia uwezo wa timu na maliasili watu (wapenzi,washabiki). Huwezi kuipa mgawo sawa timu ya Yanga na timu nyingine ambazo katika mechi zao binafsi wanatapata washabiki 50 kwenye mchezo, wakati Yanga imeongoza kwa mapato katika msimu mzima wa Ligi Kuu ya Vodacom na wastani wa washabiki 8,000 kwa kila mchezo. Mwisho Makele amesema wanauamini uongozi uliopo na wapo nao bega kwa bega, tunaomba jamii nzima itambue kuwa Yanga inapigania haki zake na hao wote wanaobeza msimamo wetu basi wajibu hoja kwa hoja na sio kuongea tu pasipo kujibu hoja. |
Wednesday, July 31, 2013
Matawi ya Yanga yaunga mkono maamuzi ya uongozi wa klabu kutoonesha live mechi za ligi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment