Thursday, February 13, 2014

Fainali ya Copa Del Rey ni El Clasico

Fainali ya kombe la ligi nchini Hispania (Copa del Rey) inatafanyika tarehe 19 April 2014 na safari hii itawakutanisha vigogo wa La Liga Real Madrid na Barcelona. Mechi hii inatarajiwa kuwa ni ngumu na kuvutia kwani Madrid na Barca ni wapinzani wa jadi nchini Hispania na ikizingatiwa pia makocha wa timu hizi wote ni wageni na wanahitaji kutwaa vikombe wakiwa na timu zao mpya. Real Madrid imefika fainali baada ya kuwafunga Atl. Madrid kwenye nusu fainali kwa jumla ya magoli 5-0, wakati Barcelona wameitoa klabu ya Real  Sociedad kwa jumla ya magoli 3-1. 




No comments:

Post a Comment