Tuesday, July 16, 2013

Shujaa wa ziara ya Arsenal nchini Vietnam

Wakiwa katika ziara nchi Vietnam, wachezaji na viongozi wa klabu ya Arsenal leo walikutana kijana mmoja ambaye wamemuita ni shujaa wa ziara yao kutokana na ujasili aliouonesha. Ujasili wa kijana huyo umekuja baada ya kukimbia umbali mrefu akilifukuza basi lililowabeba wachezaji wa Arsenal huku akiruka vichaka, kukwepa magari na pikipiki ilimradi tu awe sambamba na basi. Tukio hili liliwavutia wachezaji na viongozi wa klabu ya Arsenal na ikabidi wamuombe dereva wa basi asimame ili kijana huyo aingie ndani. Dereva wa basi alisimama na kijana aliingia ndani ya basi na aliweza kupiga picha na kila mchezaji wa Arsenal kabla ya kukabidhiwa jezi maalumu iliyosainiwa na wachezaji wote kama shujaa wa klabu hiyo kwenye ziara yao nchini Vietnam. Huu ni mfano wa watu ambao ni Arsenal damu, anaipenda klabu kutoka moyoni. 

Angalia video ya tukio hili  


Good tempo: Arsenal players were impressed with the consistent running pace of the fan
Kijana akikimbia kabla ya kuingia ndani....duu! huyu jamaa kweli Arsenal damu
In good shape: Arsenal players were impressed with the fan's six-pack as his shirt was passed round to be signed
Baada ya kuingia ndani, hapa alikuwa anapiga picha na wachezaji huku jezi yake akisainiwa na wachezaji 
Start of a signing spree? Manager Arsene Wenger signs the fan's shirt
Arsene Wenger akipiga saini yake kwa shujaa wa ziara 
Keeping the pace: Arsenal's Mikel Arteta poses with 'The Running Man' on the Gunners team coach
Shujaa akiwa na Arteta...hakika leo ametimiza ndoto zake 
On board: The fan was invited on to the team bus after his running exploits

No comments:

Post a Comment