Beki mpya wa Liverpool, Kolo Toure amemshauri mshambuliaji wa klabu hiyo Luis Suarez asihame akiamini kuwa vitu vyote anavyohitaji atavipata akiwa Liverpool. Toure aliyasema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tokea ahamie Liverpool akisema ‘ Suarez ni mchezaji mzuri, nimeshawahi kupambana naye, ni mchezaji mgumu kumkaba, nilipenda kumuona yupo upande wetu. Najua anahitaji kushinda vikombe ili afurahie maisha yake ya soka, lakini kila kitu anachohitaji atakipata akiwa Liverpool na sio klabu nyingine yoyote anayotaka kwenda. Mimi naamini ataendelea kubaki Liverpool kwa msimu ujao tukiwa pamoja na vyote anayohitaji tutavipata’. Suarez hadi sasa anahitajika na klabu tatu, Arsenal, Real Madrid na PSG na sababu kubwa ya kutaka kuhama ni kukwepa waandishi wa habari na nia ya kucheza klabu bingwa Ulaya (Uefa Champions). Arsenal imeshatoa ofa ya Euro mil 30 wakati Real Madrid wapo tayari kutoa Euro mil 38.
No comments:
Post a Comment