![]() |
Picha hii ya video imeripotiwa na vyombo vingi vya habari nchini Hispania na Uingereza wakisema Xavi alikuwa hana imani na Ramos katika upagaji penati ndiyo maana aliamua kufunika macho ili asione penati hiyo. Picha ya juu na chini inaonesha tukio hilo (Xavi akiwa amefunika macho wakati Ramos anapiga penati, kama vile alijua kuwa atakosa). Ramos ni mpigaji mzuri wa penati lakini sio mpigaji wa kwanza kwa timu ya Taifa na klabu yake, hadi sasa haijajulikana kwanini kwenye mechi hii na Brazil alipewa kupiga wakati wapigaji wakuu wa penati wa Hispania ni Torres na Xavi. Inafurahisha sana kama kweli Xavi alifunika macho ili asione penati ya Ramos. |
Monday, July 1, 2013
Xavi alifunika macho ili asione penati ya Ramos
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment