Mshambuliaji mpya wa klabu ya Man utd Wilfried Zaha leo ameonesha ugeni na aibu kiasi flani baada ya kutokea kwenye uwanja wa ndege akiwa tofauti na wenzake. Zaha alikuwa amevaa t-shirt&jinsi na chini alikuwa amevaa raba za Nike ambazo zimeripotiwa kuwa zilikuwa chafu. Zaha alitakiwa avae suti nyeusi sawa na wenzake. Lakini yeye alikwenda airport amevaa casual licha ya kuwa alijulishwa kuvaa suti. Baada ya kuwasili airport, kuulizwa suti ipo wapi alisema ameipoteza. Kufuatia hali hii, ilibidi maofisa wa Man utd wakamtafutie suti nyingine fasta fasta ili aweze kuvaa sare na wenzake....daaah!! mshikaji alishazoea Crystal Palace...hata Taifa stars sasa hivi wanavaa suti wakisafiri.
Cheki raba aliyovaa Zaha..haha daah!! huyu jamaa alikuwa anataka kuuza stori hakuwa serious
Picha hii ni baada ya Zaha kupewa suti nyingine
Wacheki wenzake walivyotokelezea na suti
Klabu ya Man utd imelekea Bangkok nchini Thailand kuanza ziara yake ya Asia kucheza mechi za kirafiki kabla ya msimu ujao kuanza. Tarehe 13 mwezi huu Man utd watacheza na Singha All-Star XI ikiwa ni mechi ya kwanza ya kocha mpya David Moyes.
No comments:
Post a Comment