Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez amekaririwa na waandishi wa habari akitaja baadhi ya makubaliano ya siri yaliyokuwepo kati yake na klabu ya Liverpool. Suarez alitaja makubaliano hayo kwa kusema ' Mimi na klabu ya Liverpool mwaka jana tulikubalina kuwa, nitahama kama Liverpool itashindwa kuingia kwenye Uefa Champions msimu ujao, na pili klabu itakayoninunua itatakiwa kulipa zaidi ya paundi mil 40. Lakini nashindwa kuelewa kwanini Liverpool haitaki kutimiza kilichopo kwenye makubaliano yetu, mimi nitakwenda kwenye mahakama ya FA ili kufungua hii kesi, lakini sipendi yafikie huko kwasababu napenda kuondoka kwa amani'. Suarez amefikia uamuzi huu baada ya Liverpool kukataa ofa ya tatu ya Arsenal ya paundi mil 40.1, ambayo ni zaidi ya ile iliyopo kwenye makubaliano. Wakati Suarez akisema hayo, kocha wa Liverpool Brendan Rodgers, amesema 'Liverpool imeitolea nje ofa ya Arsenal kwasababu haifanani na thamani ya Suarez na hatuwezi kumuuza mchezaji mzuri kama Suarez kwa wapinzani wetu'. Mgogoro huu kati ya Liverpool na Suarez haujajulikana utakwisha lini, kwani Suarez anashinikiza kuondoka kwa paundi mil 40.1 na klabu ya Liverpool inahitajia dau la Arsenal liongezeke, wakati klabu ya Arsenal imesema ofa iliyotoa imefikia mwisho wao. |
Wednesday, August 7, 2013
'Liverpool haitekelezi tulichokubaliana' Suarez
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment