Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, akisikiliza maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa teknolojia ya goli ambayo inatarajia kuanza kutumika msimu ujao wa ligi. Teknolojia hii itahusisha, mpira, saa, goli, na kamera zenye vifaa maalumu vya kuwasiliana ili kutambua goli. Teknolojia hii imegharimu kiasi cha paundi 250,000 kwa kila kiwanja, ambapo viwanja vyote vitakavyotumika kwa mechi za ligi kuu England vimeshafungwa sambamba na viwanja vitakavyotumika kwa michuano ya FA na ngao ya hisani. |
Huu ni mpira uliovuka msitari wa goli huku saa ikionesha goli. Kila mwamuzi atavaa saa hii na atakuwa akiiangalia kutambua kama ni goli. Saa hii pia itavaliwa na waamuzi wasaidizi na waakiba. |
Sensa zilizofungwa kwenye uwanja wa klabu ya Arsenal Emirates zitakazotumika kwenye teknolojia ya goli |
Chumba cha kuongozea |
Arsene Wenger akiongea na waandishi wa habari baada ya kupata mafunzo na kujionea utatendaji wa teknolojia hiyo ndani ya uwanja wa nyumbani wa Arsenal. Wenger ameonesha kuikubali teknolojia hii na amesema itatatua migogoro mingi ya magoli iliyokuwepo siku za nyuma. |
No comments:
Post a Comment