Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi akiwasili mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili ya kukwepa kodi kutokana na mapato yake ya mwaka 2006 hadi 2009. Kesi hii ilianza kusikilizwa miezi iliyopita, leo tena imeendelea na taarifa zinasema kesi hii inatarajiwa kumalizika kwani Messi mwenyewe ameshalipa kiasi cha fedha alichokuwa anadaiwa. Messi alipohojiwa kuhusiana na jambo hili alisema ' kesi inakwenda vyema, ila ukweli mimi na baba yangu hatujui kitu kwasababu masuala yote ya pesa na kodi tumewaachia mameneja wetu wa fedha na sheria. Wao wanasema kila kitu kilikwenda vyema na mambo haya yatakwisha'. Messi ameshitakiwa kukwepa kodi isiyopungua paundi mil 3.4 kutoka kwenye matangazo ya kampuni za Banco Sabadell, Danone, Adidas, Pepsi-Cola, Proctor and Gamble na kuwait food company.
|
No comments:
Post a Comment