Lionel Messi akikatisha pembeni ya kocha wake huku akiwa ameuchuna kuonesha hasira zake baada ya kufanyiwa mabadiliko katika dakika ya 80 ya mchezo kati ya Barcelona na Real Sociedad. Kocha wa Barca Tata Martino amekuwa akiwafanyia mabadiliko wachezaji wote wa Barcelona ili kuwapa nafasi wachezaji wengine kucheza, lakini zoezi hili limeonekana chungu kwa Messi baada ya kuonesha sura ya kutofurahishwa na kitendo cha kocha wake kumtoa kabla ya mchezo. Mara kadhaa Messi amekuwa akionesha hasira anapotolewa hata kwa makocha waliopita kutokana na kile alichokieleza kuwa anapenda kucheza kwenye mechi zote kwa dakika 90, kwani furaha yake ni kucheza sio kuangalia mpira. Angalia video iliyopo hapo chini kuona Messi alivyomchunia kocha wake.... |
No comments:
Post a Comment