Wachezaji wa Chelsea wakicheza mpira wa mikono ikiwa ni aina mpya ya mazoezi kufanyika tokea Jose Mourinho ajiunge na Chelsea msimu huu. Mazoezi haya mapya yalijumuisha mpira wa mikono (handball) na mpira wa kikapu (Basketball) kwa wachezaji wote wakiwemo magolikipa. Mourinho alisema amewapa wachezaji wake mazoezi haya ili wafurahi na kufanya mazoezi yawe kivutio kwa kila mchezaji na kuwajenga wachezaji kisaikolojia.
|
Picha hii inamuonesha mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich (kulia) akitoka kiwanjani akiwa hana furaha siku Chelsea ilipofungwa goli 2-1 na Basel kwenye michuano ya Uefa Champions. Kitendo klabu ya Chelsea kufungwa na Basel kwenye uwanja wa nyumbani kimemfanya Abramovich pamoja na washabiki wengi wa Chelsea kupata wasiwasi wa kiutendaji wa kocha mpya Jose Mourinho. Wasiwasi huu wa washabiki na wadau wa Chelsea ndiyo umemfanya Jose Mourinho abadilishe aina ya mazoezi. Mbali ya kubadilisha aina ya mazoezi, pia kuna uwezekano mkubwa kikosi cha kwanza cha Chelsea dhidi ya Fulham kwenye mchezo unaokuja kinaweza kubadilika na kuwapa nafasi zaidi wachezaji waliozoeleka akiwemo Mata, Mikel na Ramires.
|
No comments:
Post a Comment