Hizi ni picha nne zinazoonesha sura mpya ya kiwanja cha Real Madrid, Santiago Bernabeu kitakavyokuwa baada ya kufanyiwa matengenezo. Picha hizi nne zimewasilishwa kwa Rais wa Madrid, Perez, na wasanifu tofauti ikiwa kama mapendekezo, ambapo ni pendekezo moja tu litakalochaguliwa. Perez amesema uamuzi wa kuitengeneza upya Santiago Bernabeu ni kukifanya kiwanja kiwe na sura mpya inayoendana na karne ya 21, na matengenezo yataanza mara moja baada ya msimu huu kumalizika.
No comments:
Post a Comment