Jose Mourinho akiwa uwanjani jana usiku kuangalia mechi kati ya Belgium na Colombia. Mourinho alikwenda uwanjani kuangalia mechi hii ili kumtathimini vyakutosha mshambuliaji wa Colombia na Monaco, Falcao, ambapo katika mchezo huu Falcao alionesha mchezo mzuri na imeaminika kwa namna yoyote ile Mourinho atakuwa ameridhika na kiwango chake. Tetesi zilizopo ni kuwa Chelsea ipo tayari kulipa kiasi chochote cha pesa kumsajili Falcao kwenye dirisha dogo. Matokeo ya mwisho ya mchezo huu, Colombia walishinda magoli 2-0, magoli yakiwa yamefungwa na Falcao na Ibarbo.
No comments:
Post a Comment