Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba imetangaza kumsimamisha kazi mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Aden Rage kwa kile kilichotajwa ni kutokuwa na imani naye. Mbali ya Rage, kamati hiyo imewafukuza kazi kocha wa klabu hiyo Abdallah Kibaden na msadizi wake Julio. Kamati hiyo ya Simba imesema kutakuwa na kikao kingine tarehe 1 Desemba, kikao ambacho kitafanya maamuzi ya kudumu kulingana na mwenendo wa klabu hiyo.
Selemani Matola ndiye kocha msadizi mpya aliyeteuliwa na kamati ya utendaji ya Simba baada ya Kibaden na Julio kufukuzwa kazi.
No comments:
Post a Comment