Mmiliki wa klabu ya Liverpool, John Henry amesema atatuma ndege yake binafsi iende nchini Uruguay kumchukua mshambuliaji wa klabu hiyo Luis Suarez mara tu atakapomaliza kuichezea nchi yake. Henry amesema uamuzi wake wa kutuma ndege ni kutaka kumuwezesha Suarez kuwahi kurudi England ili aweze kupata muda wa kutosha kujiandaa na mechi ya ligi kati ya Liverpool na Everton (Merseyside derby). Uruaguay itacheza leo alfajiri dhidi ya Jordan kwenye mechi ya marudiano kufuzu kombe la dunia. Liverpool inatarajia kushuka dimbani kucheza na Everton jumamosi ya wiki hii, mechi ambayo inatarajiwa kuwa ngumu na yenye mvuto kutokana na uhasimu uliopo baina ya timu hizi.
Mmiliki wa Liverpool John Hery
No comments:
Post a Comment