Wednesday, December 18, 2013

Liverpool yampa mkataba mnono Suarez

Bbm9D4BCMAAv4l1 Liverpool offer Luis Suarez £200k a week contract to stay at Anfield [Times, Telegraph & Guardian]
Klabu ya Liverpool imempatia ofa nyingine mshambuliaji wake Luis Suarez yenye mkataba mnono wa malipo ya paundi 200,000 kwa wiki. Mkataba huo kama utakubaliwa na Suarez utamfanya aendelee kubakia Anfield kwa miaka mingine miatano baada ya 2016. Mkataba wa sasa wa Suarez unakwisha mwaka 2016 na una malipo ya paundi 130,000 kwa wiki. Mazungumzo ya mkataba mpya bado yanaendelea kati ya Mkurugenzi mtendaji wa Liverpool Ian Ayre na wakala wa Suarez ambaye ni Pere Guardiola. Liverpool imechukua uamuzi huu ili kuepuka mchezaji huyu kuhamia Arsenal au Madrid kwenye dirisha dogo. 

Pichi hii inaonesha maneno aliyoyaandika Suarez kwenye karatasi ya mshabiki mmoja wa Liverpool akisisitiza kuendelea kubakia ndani ya klabu ya Liverpool kwa miaka mitano
Bbspn7gCAAE2uI  A Liverpool fan gets Luis Suarez to sign a new five year contract to stay at Anfield [Picture]

No comments:

Post a Comment