Monday, December 16, 2013

Presha za kumsajili Suarez zimeanza tena

Baada ya klabu ya Arsenal kuangukia mikononi mwa Bayern Munich kwenye 16 bora ya michuano ya Uefa Champions, presha za usajili wa mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez zimeanza tena ndani ya klabu ya Arsenal. Hali hii imekuja baada ya kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kukiri kuwa anamuhitaji mshambuliaji huyu mapema iwezekanavyo. Wenger ameeleza hayo alipokuwa akihojiwa na Telefoot. Mbali ya kuonesha kumuhitaji Suarez, Wenger pia alimsifia mchezaji huyu kwa kila namna. “ Nafikiria kila beki hapendi kumkaba Luis Suarez, kwasababu ni mchezaji ambaye ni vigumu kumzuia. Ni mchezaji mwenye nguvu na ari ya kushambulia. Kwa taarifa nilizopewa, Suarez ni mtu rahisi sana kuishi naye na kufanya naye kazi. Pia nimeambiwa Suarez anajiheshimu na anapenda kufanya mazoezi. Ndani ya klabu ya Arsenal wote tunatamani kuwa na mchezaji kama yeye hasa kwa muda kama huu”, hayo ni maneno ya Arsene Wenger. Msimu wa usajili wa dirisha dogo unatarajia kuanza mwezi January na kama klabu ya Arsenal itafanikiwa kumsajili Suarez, basi itaweza kupambana vilivyo na Bayern Munich, klabu ambayo inapewa nafasi kubwa ya kutetea kombe la Uefa champions.  

Deft touch: Suarez scored his second and Liverpool's fourth with five minutes left

No comments:

Post a Comment