
Mchezaji wa kiungo cha kati, wa Manchester City Samir Nasri, atafanyiwa uchunguzi zaidi wa jereha la goti alilopata wakati wa mechi ya klabu hiyo dhidi ya Newcastle. Nasri aliondoshwa uwanjani baada ya kufanyiwa rafu mbaya na Mapou Yanga wakati wa mechi baina ya timu hizi mbili, ambapo Man city walishinda mabao mawili kwa nunge. Majeraha haya yatamfanya Nasri akae nje kwa wiki nane, hivyo kupelekea kukosa mechi kadhaa za ligi kuu pamoja na Uefa Champions ambazo ni dhidi ya Chelsea, Man utd na Barcelona.
No comments:
Post a Comment