Waimbaji maarufu duniani wa nyimbo za Pop, Pitbull, Jennifer Lopez na Claudia wamepewa ruhusa na shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA kuimba wimbo wa kombe la dunia litakalofanyika nchini Brazil mwaka huu. Waimbaji hawa wanatarajiwa kuimba wimbo maalum utakaopigwa siku ya ufunguzi, wakati wa mashindano na mwisho wa mashindano. Wimbo huo unatarajiwa kutolewa hivi karibuni ili uanze kuzoeleka na kupendwa kabla ya michuano. Wimbo wa WakaWaka wa Shakira ndiyo uliotumika kwenye kombe la dunia nchini Afrika ya Kusini mwaka 2010, je Pitbull na Jlo watamfunika Shakira?? Tungojee kuusikia "We are One" (Ole, Ola) ambao ni wimbo wa Pitbull na Jlo. Wawili hawa wameshawahi kutoa vibao mbalimbali kwa pamoja ambavyo vilivuma sana ikiwemo "On the floor" na "Live it up".
No comments:
Post a Comment