Ronaldo akifuta machozi mbele ya umati wa watu walikusanyika kwenye tuzo za FIFA. Alichokisema Ronaldo mbele ya umati baada ya kupokea tuzo ya Ballon D'or mwaka 2013. "Hakuna maneno ninayoweza kutumia kuelezea hisia zangu za sasa. Napenda kuwashukuru watu wangu wote wa karibu walioniewezesha kufikia hapa, Real Madrid, timu yangu ya Taifa (Ureno) na familia yangu. Wale wanaonijua mimi watakubaliana na mimi kuwa watu wengi wameniwezesha kushinda tuzo hii akiwemo pia maneja wangu, Rais wa Madrid, bila kuwasahau Eusebio, mchumba wangu na mtoto wangu". Hii inakuwa ni tuzo ya pili ya CR7 kuichukua baada ya ile ya mwaka 2008.
Tuzo ya mwaka 2013 na kulia ni tuzo ya mwaka 2008
Ronaldo akimpa mtoto wake tuzo aishike
Pele alipata tuzo ya mchezaji bora wa karne ya 20. Pele pia alitoa machozi kwa kushinda tuzo hii akisema 'nilikuwa nimeshinda vikombe vyote duniani katika kipindi changu chote nilichocheza mpira, lakini tuzo hii ya mchezaji bora wa FIFA sikuwahi kushinda kwasababu miaka yetu kulikuwa hakuna hii tuzo. Nilikuwa nawatamani sana wachezaji wasasa wanavyoshinda tuzo hii, nilitamani kuwa mimi, lakini leo nimeipata nimefurahi sana na nimekuwa mkamilifu kwa sasa".
Kikosi bora cha FIFA mwaka 2013
Manuel Neuer (Bayern Munich); Dani Alves (Barcelona), Thiago Silva (Paris St Germain), Sergio Ramos (Real Madrid), Philipp Lahm (Bayern Munich); Andres Iniesta (Barcelona), Xavi (Barcelona), Franck Ribery (Bayern Munich); Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Zlatan Ibrahimovic (Paris St Germain), Lionel Messi (Barcelona)
Zlatan Ibrahimovic ashinda tuzo ya goli bora la mwaka, cheki video ya goli. Sweden vs England.
Jupp Heynckes kocha wa zamani wa Bayern Munich ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka 2013
Katikati ni Mjerumani Nadine Angerer aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora wa soka kwa wanawake mwaka 2013
No comments:
Post a Comment