
Seydou Keita (34) amejiunga na klabu ya Valencia akitokea klabu ya Dalian Aerbin FC ya China. Keita ataichezea Valencia hadi mwisho wa msimu huu.

Adel Taarabt amejiunga na klabu ya Ac Milan kwa mkopo akitokea QPR licha ya kuwa alikuwa akicheza Fulham kwa mkopo.

Klabu ya Man utd bado ipo kwenye mazungumzo muhimu na klabu ya Bayern Munich kuhusu Toni Kroos. Marca linaripoti kuwa wajumbe wa Man utd tayari wapo nchini Ujerumani kukamilisha maongezi ya uhamisho huu kabla ya dirisha kufungwa. Pep Guardiola ameshakiri kuwa Bayern Munich ipo kwenye mazungumzo na Man utd kuhusu Toni Kroos. Taarifa zinasema pesa ya uhamisho ndiyo kikwazo hadi sasa ambapo paundi mil 25 wanazohitaji Munich zimeonekana kuwa nyingi kwa Man utd. Lakini tetesi zinaonesha klabu hizi mbili zitakubaliana punde kabla ya wikiendi.

Klabu ya Arsenal imekataliwa kumsajili kwa mkopo winga wa Barcelona, Cristian Tello (wakulia kwenye picha). Kauli hiyo imetolewa na kocha wa Barcelona Tata Martino akisema ' timu yangu imejitosheleza hakuna mchezaji atakayeondoka ndani ya dirisha dogo'. Kauli hii imemfanya Wenger kuendelea kushinikiza usajili wa mshambuliaji wa Schalke, Julian Draxler ili kuziba mapengo ya majeruhi aliyonao hivi sasa. Maongezi kati ya Arsenal na Schalke bado yanaendelea na taarifa za Sportsmail zinasema huenda Draxler akatangazwa wakati wowote kuanzia sasa kuwa mchezaji wa Arsenal. Arsenal watalipa jumla ya paundi mil 37 kumsajili Draxler. Arsenal pia wameshatajwa kufanikisha uhamisho wa mshambuliaji wa Juventus, Mirko Vucinic na imesemekana mchezaji huyu kwasasa anaelekea jijini London kufanyiwa vipimo.

Julian Draxler

Mirko Vucinic
No comments:
Post a Comment