Taarifa kutoka Sportsmail zinasema, kocha wa Man utd David Moyes wiki hii alikutana na mkuu wa kitengo cha usajili wa klabu ya Juventus ili kuongelea usajili wa wachezaji wawili Paul Pogba (kushoto) and Arturo Vidal (kulia). Moyes alifanya kikao na Juventus baada ya mechi kati ya Cagliari vs Juventus kuisha jumapili iliyopita. Matokeo ya mazungumzo haya ya awali yanasema Juventus inaweza kuumuza Pogba kwa United ndani ya dirisha dogo, lakini Vidal ataweza kuondoka mwishoni mwa msimu. Mazungumzo haya bado yanaendelea na taarifa zaidi zinatarajiwa kuendelea kutolewa. Wachezaji hawa wote wanacheza kwenye nafasi ya kiungo na ndiyo chachu kubwa ya ushindi kwa klabu ya Juventus wakisaidiana na Pirlo.
Moyes akiwa uwanjani nchini Italia kuwaangalia Pogba na Vidal jumapili ya wiki hii
Klabu ya Chelsea imefikia hatua za mwisho kumsajili kiungo wa Benfica, Nemanja Matic kwa dau la paundi mil 25. Usajili wa mchezaji huyu unatarajiwa kukamilika wiki hii baada ya kufanyiwa vipimo na kusaini mkataba. Matic ni raia wa Serbia alishawahi kuichezea Chelsea, lakini aliuzwa Benfica wakati wa dili la kumsajili David Luiz. Jose Morais ambaye ni msaidizi wa Mourinho, jumapili iliyopita alikwenda nchini Ureno kuangalia mechi kati ya Benfica na Porto ili kumcheki vyema Matic. Morais alitoa lipoti nzuri juu ya mchezaji huyu jambo ambalo limewezesha usajili wake kufikia hatua nzuri hadi sasa.
Klabu ya West Ham ipo kwenye hatua za mwisho kumsajili beki wa Man city, Joleon Lescott. Awali, West Ham walikuwa wamchukue Lescott kwa mkopo, lakini Man city waligoma jambo ambalo limeifanya klabu hiyo kujikusanya ili kulipa kwa cash.
Baada ya tetesi kuvuma kuwa kocha wa zamani wa Tottenham AVB atahamia AC Milan, wiki hii tetesi hizo zimehamia kwa mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Clarence Seedorf. Seedorf aliyeichezea Milan kwa muda mrefu, ametajwa na Skysport kuwa ni moja ya makocha wanaochukunguzwa na jopo la wataalam wa klabu hiyo ili kuweza kuchukua mikoba ya Massimiliano Allegri ambaye ameshindwa kazi mwaka huu.
Klabu ya Cardiff city ipo mbio kumchukua kwa mkopo beki wa Man utd, Fabio ndani ya dirisha dogo la usajili. Kocha mpya wa Cardiff, Ole Gunnar Solskjaer ambaye ni mchezaji wa zamani wa Man utd ndiye mshawishi mkubwa wa uhamisho huu ili aweze kuimarisha kikosi chake. Mbali ya Fabio ambaye hana namba ya uhakika kwenye kikosi cha Moyes, pia Zaha anatarajiwa kwenda Cardiff kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.
Mchezaji wa zamani wa Barcelona, Aric Abidal amemwambia Victor Valdes kuwa yupo huru kujiunga na Monaco baada ya mkataba wake kuisha. Valdes ambaye mkataba wake na Barcelona unakwisha mwisho wa msimu huu, amesema atahama Barca na kujiunga na klabu nyigine. Hadi sasa klabu ya Monaco ndiyo ipo mstari wa mbele kwenye harakati za kumsajili kipa huyu sambamba na klabu za Arsenal, Man city na PSG.
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema kwasasa hana mpango wa kusajili mchezaji yoyote kwani wachezaji wake wengi waliokuwa majeruhi wameshapona."Tulikuwa tufanya usajili mapema sana ndani ya dirisha dogo, lakini ujio wa wachezaji walikuwa majeruhi umetupa nguvu na kwasasa timu yetu ipo kamili. Gerrard na Sturridge wamesharudi dimbani na wapo fiti sambamba na Sakho tunayemtarajia kurudi wiki ijayo. Majeruhi wengine wanatarajiwa kurudi hivi karibuni na tunaamini wataimarisha zaidi kikosi chetu. Kama hali itakwenda vibaya tofauti na tulivyotarajia tutafanya usajili ndani ya dirisha dogo lakini sio jambo ambalo tunalitarajia". Hayo ni maneno ya Rodgers kuhusu usajili wa Liverpool.
No comments:
Post a Comment