

Picha hizi zinawaonesha Flamini na Wilshere wakibishana kwa hasira kuhusu jambo ambalo halikujulikana mara moja. Pembeni ni Sagna akijaribu kumvuta Wilshere ili mzozo baina yao usifikie hatua ya kupigana kwenye kiwanja cha mazoezi leo asubuhi. Kabla ya kugombana na Wilshere, Flamini pia alipishana maneno na Ozil ndani ya uwanja kwenye mechi kati ya Arsenal na Bayern Munich. Baada ya tukio hili uwanjani washabiki wengi walijua Ozil ndiye alikuwa na hasira kutokana na stresi za kukosa penati, lakini hatua ya Flamini kugombana na Wilshere imeonekana kuwa Flamini ndiye mtata na mtu mwenye hasira. Vitendo hivi vya kinidhamu kwa wachezaji vitamfanya kocha Wenger azidi kuchanganyikiwa kwani hadi sasa bado anashughulikia utovu wa nidhamu wa Olivier Giroud ambaye wiki iliyopita alitoka na mwanamke mwingine.

Wilshere akiwa na sura ya hasira huku akimwangalia Flamini (hayupo pichani)

Wilshere akiondoka mazoezini baada ya kupishana maneno na Flamini

Flamini akibishana na Ozil kwenye mechi dhidi ya Munich.
No comments:
Post a Comment