Klabu ya Arsenal imeingia kwenye awamu ya tatu ya mazungumzo na beki wa kulia Bacary Sagna ili kuongeza mkataba wake. Sagna ameshakataa mara mbili mikataba aliyopewa na Arsenal ambayo ilikuwa na kiwango kidogo cha mshahara tofauti na anavyohitaji. Sagna anahitaji mkataba wa miaka mitatu wenye malipo ya paundi 90,000 kwa wiki, wakati klabu ya Arsenal imempatia mkataba mpya wa miaka miwili na malipo ya paundi 60,000 kwa wiki. Taarifa za Sportsmail zinasema wakala wa mchezaji huyu hatakubali mkataba wowote wa Arsenal wenye malipo chini ya paundi 90,000 kwa wiki. Klabu ya Arsenal imekuwa ngumu kuongeza malipo ya Sagna kutokana na umri wake kuwa mkubwa (miaka 31) jambo ambalo wanaamini mchezaji huyu hataweza kudumu kwa zaidi ya misimu miwili akiwa na kiwango cha sasa. Sagna amekuwa na kiburi cha kugomea mikataba aliyopewa na Arsenal kutokana na maombi aliyopokea kutoka klabu nne kubwa zinazomhitaji ambazo ni PSG, Inter Milan, Monaco na Galatasaray. Kiburi kingine cha Sagna ni nfikra kuwa kwasasa klabu ya Arsenal haina beki wa kulia anatakayeweza kuziba vyema nafasi yake, hivyo kwa vyovyote vile klabu ya Arsenal itakubaliana na mahitaji yake. Arsenal wameshaanza mazungumzo na wakala wa Sagna na wanatarajia kumpa mkataba wa tatu wenye ongezeko la malipo ndani ya wiki hii na matumaini ni kufikia makubaliano.
No comments:
Post a Comment