Roberto Soldado mshambuliaji wa Valencia na Hispania, jana alipewa nafasi ya kuichezea timu ya taifa kwa mara ya kwanza dakika 90 na aliweza kuonesha mchezo mzuri. Soldado anacheza kama mshambuliaji wa mwisho (namba 9) amekuwa akifanya vizuri akiwa na klabu yake Valencia lakini bado alikuwa hajapa bahati ya kucheza kwenye timu ya taifa kutokana na viwango vizuri vya wapinzani wake David Villa na Torres. Ila kushuka kwa viwango vya wachezaji hawa kumemfanya Soldado kupata namba ya majaribio na jana aliweza kuonesha uwezo wake wakati Hispania ilipokuwa ikicheza na Uruguay na alifanikiwa kufunga goli la ushindi na kuiwezesha Hispania kuondoka na ushindi wa goli 2-1. Soldado akiongea baada ya mechi alisema 'ninafuraha kuwepo kwenye timu ya taifa na kupata nafasi ya kucheza dakika 90, siwezi kuongelea mipango ya baadaye kama nitaendelea kuwepo kwasababu ni uamuzi wa kocha, ila binafsi nitajitahidi kucheza vizuri ili niendelee kuwepo kwenye kikosi cha kwanza'. Wiki iliyopita kocha wa Hispania alipokuwa akihojiwa kuhusu kikosi chake alisema 'kikosi changu kipo tayari kwa confederation cup, ila tatizo kubwa la Hispania kwasasa ni namba tisa (9), bado nina tafuta namba 9 ya kudumu'. Kutokana na kauli hii ya kocha Del Bosque's inaonesha chaguo lake kwasasa la namba ni Soldado na sio Villa wala Torres. |
Monday, June 17, 2013
Soldado awapiga bao David Villa na Torres
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment