Tuesday, February 11, 2014

Kocha Mash asubiri vipimo vya mwisho

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Sylvester Marsh ambaye amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) anasubiri vipimo vya mwisho ili aweze kuanza matibabu. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtoa kocha huyo nyumbani kwake jijini Mwanza na kumleta Dar es Salaam kwa lengo la kuhakikisha anapata matibabu zaidi na kwa uangalizi wa karibu. Tayari majibu ya kipimo cha kwanza yameshapatikana, hivyo yanasubiriwa majibu ya kipimo kingine ili aweze kuanza rasmi matibabu, lengo likiwa ni kubaini kitaalamu ugonjwa unaomsumbua.

No comments:

Post a Comment