Thursday, April 25, 2013

Toto African na African Lyon zimeshuka daraja

Toto African ya Mwanza na African Lyon ya Dar es Salaam, ni timu mbili za mwanzo kushuka daraka katika ligi kuu Tanzania bara. Kushuka kwa timu hizi kumekuja baada ya JKT Ruvu kushinda goli 1-0 dhidi ya Lyon katika mchezo uliofanyika kwenye kiwanja cha Chamanzi jijini Dar es salaam. Ushindi wa JKT umeiwezesha kufikisha pointi 26 ambazo haziwezi kufikiwa na Toto African na Africa Lyon hata kama watashinda mechi zao zote walizobakiza. Timu moja inangojewa kuungana na Toto African na African Lyon kushuka daraja kati ya Mgambo, Ruvu JKT na Polisi Moro.

Msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ulivyo sasa
RankTeamsPlayedWinsDrawLostGDPoints
1Young Africans2417523156
2Azam FC2314542247
3Kagera Sugar231175840
4Simba SC229941136
5Mtibwa Sugar24996336
6Coastal Union23896333
7Ruvu Shooting22868030
8JKT Oljoro247710-528
9Prisons FC246810-726
10JKT Ruvu247512-1726
11Mgambo Shooting237412-725
12Toto African2541011-1222
13Police M2331010-1019
14African Lyon245415-2019

No comments:

Post a Comment