Baada ya kufululiza kwa matokeo mabaya dhidi ya Chelsea na Norwich, kocha wa Man city, Manuel Pellegrini ameamua kuwaita mazoezini wachezaji wake wote walikuwa majeruhi na wazima ili kurudisha hali ya timu kabla ya mambo kuharibika. Man city inakabiliwa na majeruhi wengi wakiwemo wachezaji tegemezi kama Fernandinho, Samir Nasri na Sergio Aguero. Licha ya kuwa majeruhi wachezaji hawa wameonekana kwenye mazoezi leo asubuhi na wanatarajiwa kuanza kucheza hivi karibuni ili kurudisha kiwango cha timu na kuendelea kucheza kiushindani. Mechi zijazo za Man city ni dhidi ya Sunderland, Chelsea (FA), Barcelona (UEFA) na Stoke City.
No comments:
Post a Comment