Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zimewaagiza wanachama wake- vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuwapatia orodha ya klabu zote za mpira wa miguu zilizosajiliwa katika mikoa yao. Orodha hiyo inatakiwa kujumuisha namba ya usajili wa klabu, viongozi waliopo madarakani kwa sasa pamoja na mawasiliano yao (namba za simu na anuani za email) na eneo yalipo makao ya klabu husika. Kwa utaratibu huo, vyama vya mikoa vitakusanya taarifa za klabu zinazocheza ligi ya mikoa, lakini wakati huo vinatakiwa kuwasiliana na wanachama wake (vyama vya wilaya) kupata taarifa za klabu zinazocheza ligi za wilaya na baadaye kuziwasilisha TFF. Klabu ambazo taarifa zake zitakuwa hazijawasilishwa TFF hadi Agosti mwaka huu hazitaruhusiwa kushiriki ligi ya msimu wa 2014/2015 katika ngazi yoyote ile.
No comments:
Post a Comment