Friday, February 7, 2014

Tamko la Azam TV kuhusu kuonesha Live EPL

Azam TV imetoa tamko baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa watazamaji wanaotaka TV hiyo kuonesha live ligi ya England (EPL). Tamko hili limetolewa kupitia akaunti rasmi ya Facebook ya TV kama ifuatavyo; 

'Wadau punguzeni jaziba kidogo duh!kidogo kidogo mpaka tutafika.nini tatizo?EPL? Wadau wetu sisi kila siku tunasema na kuwajibu kuwa,kwa sasa,narudia tena kwa msisitizo wa herufi kubwa,KWA SASA haturushi EPL live! Lakini kutokana na maoni ya wengi humu tunalifanyia kazi.Na itawabidi muwe na subira na sisi kwani KWA SASA wenye haki na uhalali wa kurusha EPL ni DSTV pekee ambo wanahaki ya kurusha Afrika ya nchi za Ukanda wa jangwa la Sahara na Afrika Mashariki kwa ujumla na Tanzania ikiwepo. Sasa haiwezekani kukatisha au kuwanyang'anya haki hiyo kwani sheria inawalinda.Mpo??Sasa tutaipataje haki hiyo??muda ukifika nasi tutadai haki hiyo sasa hapo itakuwa mwenye kisu kikali ndiye atakayekula nyama.Na ni matarajio yetu kuwa wadau mutakuwa ni wengi vya kutosha kukidhi mahitaji, na muwe tayari kama kutakuwa na mabadiliko yoyote ikiwemo ongezeko la bei'.

'Baada ya kusema hayo, kwa wale watakaoridhika kuangalia marudio ya EPL, ndipo tunawadokeza kuangalia kupitia chaneli ya Setanta ambayo nayo ipo kwenye Azam Tv, msiyotaka si lazima sana wadau. Lakini pia hapo hapo unaweza kuangalia ligi tofauti kwa mechi za timu kubwa kubwa tumeanza kuwapa apdates kama tulivyofanya juzi ilipocheza Real Madrid'.

Hayo ndiyo maneno kutoka Azam TV, nafikiri kwamba, wadau na wapenzi wa EPL watakuwa wamepata jibu kuhusu EPL na Azam TV. Watu wengi walitarajia kuona live mechi zote za Ulaya kupitia Azam TV lakini ukweli ni kwamba kuonesha mechi live kuna haki miliki hivyo Azam TV imetoa ahadi ya kutumia kisu kikali pindi muda utakapofika wa kugombania tenda ya EPL. 

No comments:

Post a Comment