
Kiungo wa Bayern Munich, Toni Kroos ameendelea kuonesha kipaji chake baada ya jana usiku kucheza mpira safi dhidi ya Arsenal hadi kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa goli 2-0. Katika mechi ya jana Kroos aliweza kupiga pasi kamili 147 peke yake wakati timu ya nzima ya Arsenal ilipiga jumla ya pasi 158. Kiwango hiki alichoonesha Kroos kimezidi kuwavutia wengi ikiwemo kocha wa Man utd David Moyes ambaye alikwenda kuangalia mechi ya jana ili kumcheki vyema kiungo huyu. Moyes alishakutana na wakala wa Kroos nchini Ujerumani na walikubaliana kufanya mipango ya uhamisho, lakini ufinyu wa muda wa dirisha dogo ulisababisha usajili wake kushindikana. Taarifa kutoka Sportsmail zinasema, Moyes kwasasa haitaji tena kufuatilia kiwango cha mchezaji huyu kwani amesharidhika, kilichobakia ni kufanya mipango ili aweze kumsajili mwishoni mwa msimu kabla ya kombe la dunia. Katika mchezo wa jana Kroos ndiye alifunga goli la kwanza kwa Munich na ndiye aliyekuwa man of the match.

Moyes akiwa Emirates jana usiku

Picha hii inaonesha mipira yote aliyoicheza Kroos dhidi ya Arsenal
No comments:
Post a Comment