Friday, March 14, 2014

Anelka kuvunja mkataba na West Brom

Strong association: Nicolas Anelka's 'quenelle' gesture is strongly associated with anti-Semitism
Nicolas Anelka ametamka kuwa hawezi kuomba msamaha kwa klabu yake ya West Brom juu ya tuhuma za kibaguzi anazoshutumiwa. Tuhuma alizopewa Anelka na klabu yake ni kuhusiana na aina ya ushangiliaji ambao klabu yake imesema unakashifu na kubagua jamii fulani ya watu. Kutokana na kufanya kitendo hicho, cha ushangiliaji kwa kuweka mkono kifuani kama ambavyo anaonekana kwenye picha, klabu yake imempa adhabu ya kukaa benchi mechi tano jambo ambalo Anelka mwenyewe amelikataa na amesema atavunja mkataba wake na West Brom kama watamlazimisha kuomba msamaha na kutumikia adhabu. 

No comments:

Post a Comment