Klabu ya Arsenal imewasili jijini Munich Ujerumani tayari kuwakabili Bayern Munich kwenye mechi ya marudiano ya Uefa champions. Klabu ya Arsenal itashuka dimbani ikiwa nyuma kwa magoli mawili baada ya kukubali kipigo kwenye uwanja wa nyumbani. Akiongea na waandishi wa habari kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema, timu yake ipo fiti kuwakabili Bayern na ana imani timu yake itasongambele kama refa atakuwa 'fair'. Wenger aliongeza kwa kusema ' historia inaonesha tumeweza kushinda mechi nyingi barani Ulaya tukiwa ugenini, hivyo sioni kama ni jambo gumu kwa Arsenal kushinda kushinda mchezo wa leo ugenini'.
Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa wa kuvutia ikikumbukwa kuwa klabu ya Arsenal ilishinda mchezo wake wa marudiano dhidi ya Bayern Munich msimu uliyopita. Lakini pia, klabu ya Arsenal imekwenda Munich ikiwa na imani kubwa ya kushinda na kutaka kuuonesha ulimwengu kuwa ina uwezo wa kuifunga Bayern Munich klabu ambayo wengi wanasema ni imara kuliko klabu zote za Ulaya. Mchezo wa leo utachezwa saa nne na dakika 45 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Mechi nyingine ya leo itakuwa ni kati ya Atl. Madrid vs Ac Milan.
No comments:
Post a Comment