Jumla ya wachezaji watatu wametajwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wapo kwenye rada ya Barcelona kusajiliwa mwishoni mwa msimu. Wachezaji hao ni David Luiz (chelsea), Jan Vertonghen (spurs) na Mats Hummels (Dortmund). Kati ya wachezaji hawa mmoja ndiye atakayeweza kusajiliwa na Barcelona ili kuziba pengo la Carles Puyol ambaye ameshatangaza kuondoka Barca kutokana na kuwa majeruhi muda mrefu. Mwishoni mwa mwaka jana Barcelona ilikuwa na nia ya kumsajili Luiz, lakini Mourinho aliweka ngumu hivyo usajili huu ulishindikana. Jambo hili linategemewa kutokea tena mwishoni mwa msimu huu kwani Mourinho na Barcelona ni maadui wa damu. Kutokana na hali hii, Barcelona wana nafasi kubwa kuwasajili Vertonghen na Hummels kuliko Luiz.
No comments:
Post a Comment