Hatimaye kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametekeleza mahitaji ya washabiki wa klabu hiyo yaliyomtaka atumie pesa nyingi alizonazo kufanya usajili kwa kumsajili Mesut Ozil kutoka Real Madrid kwa paundi mil 42.5. Usajili huu wa Ozil unavunja rekodi ya klabu ya Arsenal kwani haijawahi kutokea klabu ya Arsenal kusajili mchezaji ghali kwa kiasi hiki cha fedha. Ozil amesaini mkataba wa miaka mitano na anatarajiwa kulipwa paundi 140,000 kwa wiki |
No comments:
Post a Comment