Klabu ya Barcelona imefungiwa na FIFA kufanya usajili kwa misimu miwili baada ya kukiuka kanuni na sheria za shirikisho hilo. FIFA imesema adhabu hii inahusisha wachezaji wote ambao wapo chini ya umri wa miaka 18 kwa kipindi cha misimu miwili mfululizo. Barcelona imepata adhabu hii baada ya kufanya usajili bila kufuata utaratibu mzima wa uhamisho wa kimataifa kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2009 hadi 2013. Matokeo ya adhabu hii yataifanya klabu hii kuwatumia vijana waliopo ndani ya klabu hiyo bila kusajili wengine kwa kipindi chote cha misimu miwili ijayo na itatakiwa kufanya marekebisho ya usajili uliyokosewa ya wachezaji wote tokea mwaka 2009. Mbali ya Barcelona, shirikisho la mpira wa miguu la Hispania pia limepigwa faini ya Euro 410,000 sambamba na Euro 370,000 waliopigwa Barcelona.
No comments:
Post a Comment