Andrey Arshavin ameungana na Denilson baada ya kutemwa na klabu yake ya Arsenal ili kumpunguza mzigo kwa Arsenal. Arshavin mwenye umri wa miaka 32 ameonekana kushuka kiwango na matokeo yake amekuwa mzigo kwa klabu hiyo licha ya kwenda Zenit kwa mkopo. Arshavin tokea ajiunge na Arsenal amecheza mechi 144 na kufunga magoli 31, mkataba wake na Arsenal unatarajiwa kuisha mwezi huu Juni mwishoni na uongozi wa Arsenal umesema hautasaini tena mkataba na mchezaji huyo hivyo Arshavin ataungana na Denilson pamoja na Squaillac kuondoka ndani ya klabu. Arsenal imechukua uamuzi huu ili kutoa fursa kwa wachezaji wapya wanaotarajiwa kusajiliwa msimu huu kutoka kwenye bajeti ya paundi mil 100 ambayo Wenger amepewa kwa ajili ya usajili wa msimu huu.
No comments:
Post a Comment