Thursday, April 3, 2014

Tetesi za Hazard kuhamia PSG baada ya kuvaa jezi

Colours: Eden Hazard gave a post-match interview wearing a Paris Saint-Germain shirt
Tetesi za Hazard kuhamia PSG zilianza tokea mwezi wa kwanza mwaka huu kwenye dirisha dogo. Tetesi hizi zilikuwa zinadai kuwa Hazard atahamia PSG mwishoni mwa msimu huu. Jana usiku baada ya mechi kati ya PSG na Chelsea, tetesi hizi zilivuma zaidi kutokana na kitendo cha Hazard kuvaa jezi ya PSG wakati mchezaji huyu alipokuwa akifanya mahojiano  na Canal+ TV kama anavyoonekana kwenye picha hii. PSG kama klabu, wao walishatangaza nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyu muda mrefu, lakini Chelsea ilisema Hazard sio mchezaji wa kuuzwa. Ukweli kuhusu uhamisho huu tungojee mwishoni mwa msimu. 

No comments:

Post a Comment