Jose Mourinho anaweza kuwa kocha wa nne kumaliza msimu bila kombe kwa klabu ya Chelsea tokea Roman Abramovich aanze kuimiliki klabu hiyo. Alianza Claudio Ranieri kukosa kombe akafukuzwa kazi akifuatiwa na Carlo Ancelotti na Avram Grant. Hadi sasa klabu ya Chelsea imeshatolewa kwenye michuano yote ya ndani na nje ya England huku ikiwa nafasi ya tatu kwenye ligi kuu. Ni wazi kuwa Chelsea haitaweza kushinda kombe la ligi kuu na hivyo kumfanya Mourinho kumaliza msimu bila kombe lolote. Lakini hadi sasa hakuna fufunu zozote kuwa Mourinho atafukuzwa kazi kutokana na ugeni wake ndani ya klabu baada ya kurudi akitokea Madrid. Ukweli ni kwamba Mourinho ataendelea kuifundisha Chelsea kwa msimu mwingine zaidi ili kuirudisha klabu tena Chelsea kwenye kiwango chake kilichozoeleka. Tatizo kubwa la klabu ya Chelsea msimu huu lilikuwa ni safu ya ushambualiji na tayari Mourinho ameshaonesha nia ya kumsajili Diego Costa (Atl. Madrid) baada ya kushinda kumnasa Rooney.
No comments:
Post a Comment